Equatorial Guinea – Wote Waliorekodiwa Wanafukuzwa Kazi
Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema Serikali ya Nchi hiyo itawatimua kazini Maafisa na Watumishi wote wa Umma ambao ni miongoni mwa Wanawake zaidi ya 400 waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) la Nchini humo, Baltasar Ebang Engonga (54) katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye Ofisi za Serikali na nyumbani kwa Ebang.
SIMILAR: Baltasar Engonga na Skendo ya Video za Aibu
Ebang ambaye ni Baba wa Familia ya Watoto sita, tayari amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake hao ambao wengine ni Wake za Watu akiwemo Mke wa Kaka yake, Binamu yake, Dada wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mkuu wa Ulinzi wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Nchi hiyo na Mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nchi hiyo.
Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni Mke wa Mlinzi wake (Bodyguard), Mke wa Mchungaji wake, Wake wa Mawaziri kadhaa wa Nchi hiyo, Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa kike na Wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa.
SIMILAR: Mwanamke Ajiua Baada ya Video Kuvuja Kwenye Kashfa ya Waziri – Baltasar Ebang Engonga
Ebang Engonga ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la ANIF ambalo ni Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la Equtorial Guinea linalohusika na kusimamia uchunguzi wa kifedha na kusimamia shughuli zinazolenga kudhibiti ufisadi wa kifedha Nchini humo.
SOURCE: Millard Ayo
#kichwahitsUPDATES